karibu

aisha

printers

classic

Tuesday, November 27, 2012

PICHA ZA GARI YA SHAROBARO BAADA YA AJALI




 Msanii wa vichekesho na Muziki wa kizazi kipya nchini Hussein Ramadhani Mkiete, almaarufu Sharo Millionea, ambaye alifariki jana usiku majira ya saa mbili anatarajiwa kuzikwa kwao Mkoani Tanga mara baada ya taratibu za mazishi kukamilika.
Ajali hiyo mbaya ilitokea eneo la Maguzoni Tanga baada ya gari alilokuwa akiendesha T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza kuacha njia na kupinduka na alifariki dunia hapohapo ambapo polisi walimtambua baada ya kuona vitambulisho vyake pamoja na picha moja ya paspot size aliyokuwanayo mfuko ambapo vitu hivyo vyote viko polisi.
 Rafiki wa karibu wa Sharo Diwani Makame Seif, akieleza kwenye kituo kimoja cha radio alisema sharo Millionea ameumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono. Pia Mjomba wa marehemu amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na asubuhi ya leo ratiba ya msiba itatolewa. Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo imeshafika Hospitali ya Teule ya Tanga.
  Jana usiku majira ya saa 3:00 Kamanda wa Polisi Tanga alisema,
“leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
  Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.

No comments:

Post a Comment