SIKU chache baada ya mwigizaji mahiri Bongo, Aunt Ezekiel kuolewa kimyakimya, ndoa hiyo imepigwa zengwe kufuatia mwanaume muoaji kutoonekana kwenye tukio hilo.
Aunt Ezekiel akiwa kapozi wakati wa ndoa yake.
Aunt alifunga ndoa Oktoba 18, mwaka huu na mchumba wake wa siku
nyingi aitwaye Sunday Demonte lakini baada ya tukio hilo minong’ono ya
chinichini ilianza huku watu wakidai kuwa, kwa namna ilivyokuwa, kuna
kitu nyuma ya pazia.“Sasa ndoa gani hii mwanaume haonekani kabisa? Au ndiyo changa la macho lenyewe? Kwa ndoa kama hizi muda si mrefu utasikia kimenuka,” alisikika akisema mmoja wa wadau walioziona picha za sherehe hiyo mtandaoni.
Aidha, kuna ambao walikwenda mbele zaidi kwa kuhoji usiri uliokuwa umetawala na hata picha ambazo zinamuonesha Aunt tu akiwa kwenye mapozi.
Tabasamu la ndoa.
“Kwa ndoa ya staa kama huyu tulitarajia kuona picha za matukio
mbalimbali lakini ni tofauti, kila picha ni yeye na chache akiwa na
mashosti zake, mbona hatuoni za ndugu zake na tukio la kufungwa ndoa?”
alihoji Husna wa Kinondoni.Katika kushibisha habari hii, mwandishi wetu aliongea na Aunt ambaye alisema, ndoa aliyofunga wala haistahili kutiliwa shaka kwani mumewe yuko Dubai ila amewakilishwa na ndugu yake kwa kufuata taratibu za Kiislam.
“Ni ndoa halali kabisa na mume wangu amewakilishwa na ndugu yake ila ataungana nami kwenye sherehe kubwa itakayofanyika huko Dubai,” alisema Aunt.
..akipata maelekezo kutoka kwa Shehe.
..akisaini kitabu cha ndoa.
Source at global publishers.com
No comments:
Post a Comment